1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfghanistan

Tetemeko jengine lapiga magharibi mwa Afghanistan

12 Oktoba 2023

Tetemeko jengine kubwa la ardhi limelipiga eneo la magharibi mwa Afghanistan baada ya lile la awali kuwauwa zaidi ya watu 2,000 na kuviangamiza kabisa vijiji vya jimbo la Herat.

https://p.dw.com/p/4XRCu
Vikosi vya uokozi nchini Afghanistan vimekuwa vikiwatafuta waathiriwa baada ya tetemeko la ardhi kupiga mkoa wa Herat na kusababisha maafa makubwa.
Vikosi vya uokozi nchini Afghanistan vimekuwa vikiwatafuta waathiriwa baada ya tetemeko la ardhi kupiga mkoa wa Herat na kusababisha maafa makubwa.Picha: ranian Red Crescent Society/ZUMA/picture alliance

Tetemeko lenye ukubwa wa 6.3 kwa kipimo cha Richter lilipiga eneo lililo umbali wa kilomita 28 nje ya mji mkuu wa jimbo hilo hapo jana, na kusababisha maporomoko ya ardhi yaliyoziba njia kuu baina ya Herat na jimbo jengine la Torgondhi.

Msemaji wa serikali ya Afghanistan, Janan Sayiq, amesema hadi sasa wana taarifa za kifo cha mtu mmoja na majeruhi 120 kutokana na tetemeko hilo.

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, MSF, limesema limewapokea majeruhi 117 kwenye Hospitali Kuu ya Herat.

Nyumba 700 ambazo zilikuwa zimesalimika kwenye matetemeko yaliyotangulia, zimeangushwa kwenye tetemeko la jana katika kijiji cha Chahak.