1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran.Iran yakataa kuridhia agizo la Umoja wa Mataifa.

31 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDGO

Iran bado imeendelea kukaidi juu ya amri ya Umoja wa Mataifa licha ya kuwa siku ya mwisho ya kuridhia vivutio vya Umoja huo ili nchi hiyo kuachana na harakati zake za uzalishaji wa maadini ya Uranium ama kukabiliwa na vikwazo.

Kabla ya tarehe hii ya mwisho kumalizika, rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad amesema nchi yake haitosalimu amri kutokana na kishindo juu ya mpango wa Tehran wa nguvu za Atomik.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan amesema jitihada zinaandaliwa ili kufanyika mkutano kati ya Iran na nchi zenye nguvu za Magharibi.

Iran inadai kuwa kuzalisha kwa wingi maadini ya Uranium ni kwa matumizi ya amani hivyo taifa hilo lina haki ya kuzalisha na halita simamisha.