1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Iran iko tayari kuingia kwenye meza ya mazungumzo na Umoja wa Ulaya kuhusu mpango wake wa Nuklea

6 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFG4

Serikali ya Iran imesema inataka kuendelea na mazungumzo juu ya mpango wake wa kinuklea na Umoja wa Ulaya.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran bwana Kamal Kharazi amewaambia waandishi habari mjini NewYork nchini Marekani kwamba nchi yake imejitayarisha kufanya mazungumzo hayo ilimradi kuna matumaini ya kuyafikia makubaliano.

Iran imekubali kusimamisha kwa muda shughuli zake za kuyarutubisha madini ya Uranium kwa ajili ya kutengeneza silaha za Kinuklea lakini imetishia kurejelea upya mpango huo.

Uingereza , Ujerumani na Ufaransa zimejitolea kuishawishi Iran kwa kuihahidi kuisaidia kiuchumi na kisiasa iwapo itamaliza kabisa mpango wake huo.

Marekani imeishutumu Iran kwa kutengeneza kisiri silaha za kinuklea dai ambalo limepingwa na Iran.