1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN. Mjumbe wa Iran akutana na mkuu wa shirika la nishati la umoja wa mataifa

26 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEhR

Mjumbe wa Iran kwenye mazungumzo juu swala la kinuklia muhafidhina bwana Ali Larijani amekutana na mkuu wa shirika la kimataifa la umoja wa mataifa la kushughulikia nguvu za nishati bwana Mohamed el Baradei huku mzozo wa Iran juu ya kuendelea na mpango wake wa nuklia ukiendelea.

Bwana Larijani ametaka nchi nyingine zaidi zishirikishwe katika mazungumzo hayo badala ya Uingereza, Ujerumani na Ufaransa pekee.

Umoja wa Ulaya umekuwa ukifanya mazungumzo na Iran kwa miaka miwili iliyopita katika juhudi za kuishawishi nchi hiyo iache mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium, mpango ambao nchi za magharibi zina hofu huenda Iran ikatumia madini hayo kutengeneza silaha za kinuklia.

Mkutano wa agsosti 31 ilifutiliwa mbali wakati Iran ilipokiuka agizo la umoja wa Ulaya na kukifungua kiwanda chake cha kurutubisha madini ya Uranium.

Umoja wa ulaya sasa unataka kuipeleka Iran mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa ili iwekewe vikwazo.