1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN :Iran yashutumu Umoja wa Ulaya kwa kutokuwa makini

6 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFZC

Maafisa wa serikali ya Iran leo hii wameishutumu vikali Umoja wa Ulaya kwa kutokuwa makini katika mazungumzo yenye lengo la kupata hakikisho kwamba Jamhuri ya Kiislam ya Iran haitotengeneza silaha za nuklea.

Akikaririwa na shirika la habari la taifa IRNA mwanadiplomasia mwandamizi na msuluhishi Hossein Moussavian amelalamika kwamba Uingereza,Ufaransa na Ujerumani hadi sasa hazikuonyesha umakini wowote na kwamba Iran imekuwa na mashaka mazito juu ya uwezo wao wa kufikia muafaka katika mazungumzo hayo.

Amekaririwa akisema Iran haikushuhudia hatua yoyote ile maendeleo inayotakiwa na kuonya kwamba usitishaji wa shughuli nyeti za nishati ya nuklea wa Iran unaweza kuwa hatarini.

Wasuluhishi wa Uingereza,Ufaransa na Ujerumani wanajaribu kuishawishi Iran kuachana na mipango yake ya nishati ya nuklea ambayo Marekani inasema ni sehemu ya kutengeneza kwa siri silaha za nuklea ili badala yake Iran ipatiwe manufaa ya kiuchumi na kisiasa.