1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran yafungua mlango kwa wakaguzi wa umoja wa mataifa

2 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEMV

Iran imewaruhusu wakaguzi wa nishati ya Nuklia wa umoja wa mataifa kuzuru sehemu yenye ulinzi mkali wa kijeshi katika juhudi za nchi hiyo za kutotaka kufikishwa mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Balozi mbali mbali nchini Iran zimesema kwamba wakaguzi wa shirika la kimataifa la kudhibiti nishati ya Nuklia la umoja wa mataifa wameruhusiwa kuzuru eneo la Parchin kufanya uchunguzi iwapo Tehran ina tekeleza mpango wa siri wa kutengeneza silaha za Nuklia.

Marekani na mataifa mengine yanashuku kwamba Iran inatengeneza silaha za Nuklia kwa siri.

Sampuli mbali mbali za vyuma zimechukuliwa kutoka eneo la Parchin, kufanyiwa uchunguzi zaidi kukadiria iwapo vina chembe chembe zinazo husiana na madini ya kinuklia.