1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Tawala za kijeshi Afrika magharibi, zataka zirudishwe ECOWAS

10 Februari 2023

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa matatu ya Afrika Magharibi ambayo yalishuhudia mapinduzi ya kijeshi hivi karibuni wametoa wito wa nchi hizo kurejeshwa ndani ya taasisi mbili muhimu za kikanda.

https://p.dw.com/p/4NJoQ
Mali Oberst Assimi Goita, Anführer der malischen Militärjunta
Picha: Annie Risemberg/AFP/Getty Images

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa jana mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa ya Mali, Guinea na Burkina Faso wamesema wamefikia makubaliano ya kufanya kazi pamoja kufanikisha kurejeshwa kwa mataifa hayo kuwa wanachama wa Umoja wa Afrika na jumuiya ya kiuchumi ya ECOWAS.

Uanachama wa nchi hizo tatu ndani ya ECOWAS na Umoja wa Afrika ulisitishwa kwa nyakati tofauti kutokana na mapinduzi ya kijeshi yaliyokosolewa vikali.

Taasisi hizo mbili zinataka tawala za kiraia kurejea madarakani kama sehemu ya masharti ya kuondoa kikamilifu vikwazo na vizuizi dhidi ya mataifa hayo matatu.