1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiTanzania

Tanzania: Polisi kuwahoji watuhumiwa kwa sauti na vidio

Deo Kaji Makomba
22 Februari 2024

Makundi ya watetezi wa masuala ya haki za binadamu na wanasheria nchini Tanzania wameusifu mwongozo mpya uliotolewa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma unaoweka utaratibu wa kuwahoji watuhumiwa wa makosa ya jinai.

https://p.dw.com/p/4ckcI
Dar es salaam, Tanzania | Mkuu wa Jeshi la Polisi Camillius Wambura
Mkuu wa jeshi la Polisi Tanzania The Camillus Wambura,Picha: Ericky Boniphace/DW

Kutungwa kwa kanuni hizo kunafuatia kuwepo malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa watuhumiwa wa makosa mbalimbali wakati maelezo yanapowasilishwa mahakamani wakidai kupewa maelezo ambayo yanakuwa yameandikwa hata kabla ya kuhojiwa huku wakipigwa na kuteswa na kuambiwa kusaini ili kuthibitisha kuwa wao ndio wameyatoa.

Hatua hiyo ya Jaji mkuu wa Tanzania Ibrahimu Juma kutunga kanuni za sheria zitakazowawezesha watuhumiwa kuchukuliwa maelezo kwa njia ya sauti na vidio imepokelewa kwa bashasha na wadau wa masuala ya kutetea haki za binadamu nchini Tanzania.

Wakisema kuwa mfumo huo utafanya haki kutendeka na kupunguza vitendo vya baadhi ya polisi kuwabambikizia watuhumiwa maelezo.

Soma pia:Watetezi haki za binaadamu Tanzania watishwa

Anna Henga ni Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za haki za binadamu nchini Tanzania, anasema licha ya kanuni hiyo kutungwa lakini bado kutakuwa na changamoto katika utekelezaji.

"Bado kutakuwa na changamoto katika utekelezaji wa mfumo huo." Alisema mkuu huyo wa shirika la kutetea haki za binadamu LHRC katika taifa hilo la Afrika mashariki.

Kanuni inatokana na sheria ya makosa ya jinai

Salim Said Salim ni mwandishi habari mkonge mwenye uzoefu pia na uandishi wa habari za mahakama, amesema utaratibu wa kuchukua maelezo kwa njia ya sauti na video kutoka kwa watuhumiwa ulizingatia sheria ya makosa ya jinai.

Rais Samia:Haki kwa watuhumia izingatiwe

"Utaratibu huu umeanza kutumika baada ya jaji mkuu wa Tanzania kutunga kanuni zinazowezesha utaratibu huo, chini ya kifungu cha saba cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai marejeo ya mwaka 2022." Salim aliiambia DW.

Soma pia:Tanzania ni mkondo wa usafirishaji haramu binadamu

Sehemu ya pili ya kanuni hizo inaelekeza namna ya kurekodi mahojiano na mtuhumiwa na mazingira ya chumba yanamofanyika mahojiano kuwa eneo kubwa linalopaswa kuonyeshwa na mtuhumiwa anaporekodiwa aonyeshwe taswira yake yote.

Wafuatiliaji wa masuala ya haki za binadamu nchini humo pamoja na raia, mara kadhaa wamekuwa wakilishutumu jeshi la polisi kubambikia maelezo watuhumiwa.

Kuanza kutumika kwa mfumo huo kikamilifu kunatajwa kutakuwa na ahueni katika mfumo wa haki jinai nchini humo