1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yaidhinisha ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda

21 Februari 2023

Tanzania leo imeidhinisha ujenzi wa bomba la mafuta ghafi lenye thamani ya dola bilioni 3.5, mradi ambao tangu ulipotangazwa kwa mara ya kwanza umezusha wasiwasi juu ya masuala ya mazingira na haki za binaadamu.

https://p.dw.com/p/4NndK
Uganda Ölförderung Umwelt Indigene Total
Picha: Jack Losh

Bomba hilo litakalokuwa na urefu wa zaidi ya kilometa 1,400 litasafirisha mafuta ghafi kutoka kwenye visima vinavyoendelezwa eneo la ziwa Albert kaskazini magharibi mwa Uganda hadi kwenye bahari ya Hindi upande wa Tanzania

Ujenzi wake ulihitaji idhini kutoka mataifa yote mawili na mwezi uliopita Uganda tayari ilitoa kibali cha mradi huo kwa kampuni itakayoendesha bomba hilo ya East African Crude Oil Pipeline.

Mkuu wa kampuni hiyo nchini Tanzania amesema kutolewa kwa kibali cha Tanzania hii leo kunafungua milango ya kuanza kwa ujenzi wa  mradi huo  ambao makundi watetezi wa haki za binadamu na mazingira wanaupinga kwa madai kwamba utaharibu makaazi ya watu na ikolojia.