1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yaanza siku tatu za maombolezo ya kitaifa

11 Septemba 2011

Maombolezo yanafuatia kuzama kwa meli ya abiria mapema jana ambapo watu takriban 200 walikufa. Huku kukiwa na huzuni na kilio, watu wameghadhabishwa na ajali hiyo ambayo ingeweza kuzuiliwa

https://p.dw.com/p/12Wua
Waokoaji wakibeba maiti baada ya meli kuzamaPicha: picture-alliance/dpa

Maombolezo ya kitaifa ya siku tatu yameanza leo huko nchini Tanzania kufuatia kuzama kwa meli ambapo watu wapatao 200 walikufa. Meli hiyo ambayo kwa mujibu wa watu walionusurika wanasema ilikuwa imejaza sana abiria kupita kiwango inachotakiwa kubeba cha abiria 650, ilizama mapema jana wakati ilipokuwa ikisafiri kutoka kisiwa cha Unguja kwenda Pemba. Zaidi ya watu 600 waliokolewa, huku madarzeni ya watu wakikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Fährunglück in Tansania Afrika
Mtoto aliyekuwa miongoni mwa waliookolewaPicha: picture-alliance/dpa

Serikali imeamuru uchunguzi ufanywe kufuatia ajali hiyo, huku familia zikiendelea kuzitambua maiti za jamaa zao. Wafanyakazi wa uokozi wanaamini maiti zaidi bado zimekwama ndani ya chombo hicho kilichozama, kwa jina MV Spice Islander. Waokoaji wamerauka leo kuendelea na kazi ya kuwatafuta watu ambapo hadi sasa hawajapatikana, lakani hawatarajii ya kupata watu walionusurika.

Mwandishi: Josephat Charo/afpe

Mhariri: Mohamed Dahman