1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yafuzu kushiriki fainali za michuano ya AFCON, 2024

Lillian Mtono8 Septemba 2023

Tanzania imefuzu kushiriki fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON baada ya kumaliza ikiwa nafasi ya pili katika hatua ya makundi siku ya Alhamisi. Haya ni mafanikio makubwa kwa timu ya taifa hilo, Taifa Stars ambayo kwa mara ya mwisho ilishiriki mwaka 2019. Fainali hizi za AFCON zitachezwa huko Ivory Coast mwezi Januari 2024.

https://p.dw.com/p/4W78X