1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TAMPERE: Tatizo la wakimbizi halikusuluhishwa

22 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDAE

Mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi za Umoja wa Ulaya wameshindwa kupata suluhisho kuhusu tatizo la maelfu ya wakimbizi wa Kiafrika,wanaoingia Ulaya kupitia Hispania,Italia na Malta.Katika mkutano wa mawaziri hao mjini Tampere nchini Finland,Ujerumani imeukataa wito wa Hispania wa kutaka kusaidiwa kifedha kuwagharimia wakimbizi hao.Waziri wa ndani wa Ujerumani,Wolfgang Schäuble amesema,daima njia rahisi ni kuomba msaada wa fedha kutoka nje.Kwanza dola ambako wakimbizi huwasili,linapaswa kutekeleza wajibu wake aliongezea Schäuble.Hata hivyo Ujerumani ipo tayari kuwasaidia maafisa wa ulinzi wa mipaka wa nchi za Umoja wa Ulaya -Frontex.