1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tamasha la filamu la kimataifa la Berlinale limeanza Berlin

17 Februari 2022

Tamasha la mwaka huu ambalo ni la 72 limeanza mjini Berlin nchini Ujerumani kwa kuzingatia taratibu zote za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona. Kati ya filamu kutoka pande mbalimbali za dunia zilizoonyeshwa katika tamasha hilo lililoanza Februari 10 hadi 20, baadhi zimetoka katika nchi za Afrika.

https://p.dw.com/p/47A0e

Katika Makala ya Sura ya Ujerumani, Harrison Mwilima anaangazia filamu mbili za simulizi kutoka Afrika zilizoonyeshwa kwenye tamasha la Berlinale. Filamu hizo zinatokana na mradi unaoitwa Generation Africa au Vizazi vya Afrika wa kusaidia waandaa filamu wa Afrika kuweza kutengeneza filamu zenye viwango vizuri, zinazoweza kuonyeshwa katika matamasha ya filamu ya kimataifa.