1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taliban: yaweka zuio la kusafiri

Hawa Bihoga
28 Februari 2022

Marufuku mpya ya kutotoka nje ya Afghanistan ilitolewa na msemaji wa serikali ya Taliban Zabihullah Mujahid, Jumapili akisema zuio hilo linalenga kuwakinga waafghanistan na ugumu wa maisha wakiwa nje ya taifa hilo.

https://p.dw.com/p/47k3F
Afghanistan Sheberghan | Militärübung in Sar-e Pol
Picha: Mustafa Bag/AA/picture alliance

Uhamishwaji wa waafghanistan ulioandaliwa na mashirika ya kibinadamu au mataifa mengine umezuiliwa,na familia ambazo zinahitaji kuondoka kwa mbinu zao, zinahitaji kuwa na sababu muhimu tofauti na hivyo huzuiwa na mamlaka ya uhamiaji.

Msemaji waTaliban, Zabihullah Mujahid ameuambia mkutanbo wa wanahabari kuwa uamuzi wa kupiga marufuku raia kuondoka ulikuja kutokana na Taliban kupokea taarifa za maelfu ya Waafghanistan wanaoishi katika hali mbaya  nje ya nchi.

Ameongeza kwamba serikali ina jukumu la kuwalinda wananchi hivyo uhamishwaji utasitishwa hadi watapopata uhakika maisha yao hayapo kwenye hatari.

Vikwazo hivyo vipya vya usafiri vinaleta wasiwasi kwa  makumi ya maelfu ya Waafghanistan ambao wameahidiwa hifadhi nje ya nchi baada ya kufanya kazi na vikosi vya kigeni vilivyoongozwa na Marekani au mashirika mengine ya Magharibi wakati wa uasi wa Taliban wa miaka 20.

Taliban-Sprecher Sabiullah Mudschahid
Msemaji wa Taliban Zabihullah MujahidPicha: Xinhua /imago images

Zaidi ya waafganistan 120,000 na wale wenye uraia pacha walihamishwa hadi Agosti 31 wakati wanajeshi wa mwisho walioongozwa na Marekani walipoondoka nchini humo, wiki mbili baada ya kundi hilo lenye msimamo mkali kuteka mji mkuu, Kabul.

Aidha bado maelfu ambao nao walikuwa na dhima ya kuondoka nchini humo wamesalia Afganistan,ingawa wanatamani kuondoka lakini wanahofia kushambuliwa na Taliban.

Uhamisho rasmi wa mwisho wa kutumia ndege ulikuwa Desemba 1, ingawa wiki iliopita kulishuhudiwa misafara  barabarani ikielekea Pakistani.

Soma zaidi:Wanawake wameathirika zaidi katika utawala wa Taliban

Tangu kundi la Taliban kuchukua mamlaka  mwezi Agosti, Afghanistan imetumbukia katika mgogoro wa kiuchumi na kutoa msukumo hata kwa wale wasio na uhusiano na utawala wa zamani kutaka kuondoka.

Kila siku maelfu ya watu  hujaribu kuvuka hadi nchi jirani ya Iran kutafuta kazi, ama kwa lengo la kufika Ulaya kwa matumaini ya kupata hifadhi.

Oparesheni ya kuzuia uhalifu

Taliban control at checkpoints in Kabul
Taliban wakifanya ukaguzi kwenye magari binafsiPicha: Haroon Sabawoon/AA/picture alliance

Wakati huo huo,msako mkubwa wa usalama mjini Kabul unaendelea leo Jumatatu huku maafisa wa Taliban wakienda nyumba hadi nyumba kutafuta silaha na wahalifu wanaoshutumiwa kwa matukio ya wizi na utekaji nyara yaliyoshamiri kwa siku za hivi karibuni.

Taliban imesema kupitia msako huo mamlaka imegundua wahanga wawili waliotekwa nyara wakati wa operesheni hiyo kufikia sasa, na pia waliwaachilia wasichana wawili ambao waliwakuta wamefungwa kwa minyororo kwenye chumba cha chini ya ardhi.

Soma zaidi:Taliban wamkamata mpiganaji aliemuuwa mwanamke wa Hazara

Mujahid amewaambia wanahabari, silaha nyepesi na nzito, vilipuzi, vifaa vya redio na ndege zisizo na rubani zimekamatikana, pamoja na magari ya jeshi au serikali, katika msako huo watu sita wanaoshukiwa kuwa ni wanachama wa kundi la dola la kiislamu wamezuiliwa, watekaji nyara tisa na watu 53 wanaoshukiwa kuwa wezi.

Chanzo:AFP