1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taliban yaonya mkataba wake na Marekani unaelekea kuvunjika

6 Aprili 2020

Kundi la Taliban linasema mkataba wake wa amani waliotia saini na Marekani unaelekea kuvunjika. Kundi hilo linaituhumu Marekani kwa kukiuka mkataba huo kwa kuwashambulia raia kwa ndege zisizo na rubani.

https://p.dw.com/p/3aVHY
Russland Moskau | Sprecher der Taliban: Suhail Shaheen
Picha: picture-alliance/AP Photo/A. Zemlianichenko

Kundi la Taliban linasema mkataba wake wa amani waliotia saini na Marekani unaelekea kuvunjika. Kundi hilo linaituhumu Marekani kwa kukiuka mkataba huo kwa kuwashambulia raia kwa ndege zisizo na rubani.

Kundi hilo aidha linadai Marekani inaikosoa vikali serikali ya Afghanistan kwa kuchelewesha kuachiwa kwa wafungwa 5,000 wa Taliban kama ilivyoafikiwa katika makubaliano hayo.

Taliban imesema haifanyi mashambulizi dhidi ya vikosi vya Afghanistan na haivishambulii pia vikosi vya kimataifa mambo wanayosema hayakuainishwa wazi kwenye makubaliano hayo ya Februari.

Taarifa hiyo ya Taliban iliyotolewa jana imeonya kutakuwa na machafuko zaidi endapo serikali ya Marekani na Afghanistan wataendelea kukiuka makubaliano hayo.

Msemaji wa jeshi la Marekani kanali Sonny Leggett lakini amejibu kwa ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa Twitter akisema vikosi vya Marekani vinaendelea kuunga mkono mkataba huo.