1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Taliban yachoma moto vyombo vya muziki Afghanistan

30 Julai 2023

Polisi wa maadili wa serikali ya Taliban nchini Afghanistan wamechoma moto vyombo kadhaa vya muziki mapema leo katika mkoa wa Herat magharibi mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4UYTu
Raia aliyevunjiwa vyombo vya muziki na mamlaka za Afghanista
Raia aliyevunjiwa vyombo vya muziki na mamlaka za AfghanistanPicha: Hussein Malla/AP Photo/picture alliance

Shirika la habari la Bakhtar linalomilikiwa na serikali limemnukuu mkuu wa kukuza maadili wa mkoa huo Sheikh Aziz al-Rahman al Muhajir akisema mamlaka zimechukua hatua hiyo kwa kuwa muziki umepigwa marufuku.

Soma zaidi: Saluni, maduka ya urembo yafungwa leo Afghanistan

al Mujahir amesema muziki ni aina ya ufisadi unaosababisha vijana kupotoka na kuharibu maadili ya jamii.

Kundi la Taliban, lilipiga marufuku vyombo vya habari kupiga muziki mara baada ya kutwaa madaraka Agosti 2021. Hivi karibuni wamiliki wa kumbi za harusi pia walizuiwa kupiga muziki na kufanya shughuli zozote zinazopingana na taratibu za dini ya Kiislamu.