Taliban waua tena mjini Kabul
14 Septemba 2011Matangazo
Watu wasiopungua saba wameuawa katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul, kufuatia mashambulio kadhaa yaliyofanywa na Taliban katika mji huo.
Sehemu zilizoshambuliwa ni pamoja na ubalozi wa Marekani,makao makuu ya NATO na majengo mengine yaliyopo kati kati ya mji huo.
Washambilizi walitumia roketi za kurushia magurunedi na washambuliaji wa kujitoa mhanga walijiripua kwenye makao makuu ya polisi.
Hii ni mara ya kwanza kwa Taliban kufanya mashambulio makubwa kwa wakati mmoja katika sehemu mbalimbali ambayo ni ya pili,katika mji wa Kabul, mnamo muda usiozidi mwezi mmoja.
Msemaji wa Umoja wa Ulaya nchini Afghanistan ameungana na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton katika kuyalaani mashambulio hayo ya Taliban.
f