1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Taliban wamuua mpanga shambulizi la uwanja wa ndege wa Kabul

26 Aprili 2023

Serikali ya Taliban nchini Afghanistan imemuua mtu anayeshukiwa kupanga shambulizi la bomu lililotokea mwaka 2021 kwenye uwanja wa ndege mjini Kabul wakati Marekani ilipokuwa ikiondoa vikosi vyake.

https://p.dw.com/p/4QZBr
Afghanistan Taliban-Kämpfer in Kabul
Picha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Taarifa hizo zimetolewa na afisa mmoja mwandamizi wa serikali ya Marekani aliyezungumza na jarida maarufu la masuala ya siasa la Politico kwa sharti la kutotajwa jina.

Kulingana na afisa huyo, mtu huyo ambaye jina lake halijatambulishwa lakini alikuwa kiongozi wa kikundi kilichopanga hujuma hiyo aliuwawa na vikosi vya Taliban wiki kadhaa zilizopita.

Afisa huyo amesema hata hivyo Marekani haikuhisika kwenye operesheni hiyo.

Kwenye shambulizi hilo la Agosti 26, 2021, mshambuliaji wa kujitoa muhanga alijiripua katikati mwa umati wa watu waliofurika katika uwanja wa ndege wa Kabul wakijaribu kuikimbia Afghanistan baada ya Taliban kuchukua udhibiti wa nchi hiyo.

Watu 170 ikiwemo wanajeshi 13 wa Marekani waliuwawa.