Asili na mazingiraTaiwan
Taiwan yakumbwa na mfululizo wa matetemeko ya ardhi
23 Aprili 2024Matangazo
Mamlaka nchini humo hata hivyo zimesema hakukuwa na uharibifu mkubwa ulioshuhudiwa. Matetemeko zaidi yalisikika maeneo ya jimbo la Hualien na mji mkuu Taipei.
Soma zaidi:Mamia wahamishwa kutoka hifadhi ya taifa baada ya tetemeko Taiwan
Mnamo April 3 mwaka huu, watu 17 walikufa huko Taiwan kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 7.4 ambalo pia lilisababisha maporomoko ya udongo na uharibifu mkubwa wa majengo na miundombinu.