1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taifa Stars yatupwa nje ya michuano ya AFCON

25 Januari 2024

Timu ya taifa ya Tanzania taifa stars, imetupwa nje ya michuano ya AFCON baada ya kutoka sare tasa na Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ambayo imejikatia tiketi ya hatua ya mtoano ikiwa na alama 3

https://p.dw.com/p/4be5g
Mechi kati ya Burkina Faso na Mauritania katika michuano ya AFCON nchini Ivory Coast mnamo Januari 16, 2024
Mechi kati ya Burkina Faso na MauritaniaPicha: Kenzo Tribouillard/AFP/Getty Images

Jamhuri ya kidemokrasi ya  Kongo ambayo imetoka sare tasa na taifa stars, sasa  imejikatia tiketi ya hatua ya mtoano ikiwa na alama 3.

Katika kundi hilo F, Morocco imeifunga Zambia bao moja kwa nunge. Ushindi huo umeipatia nafasi Ivory Coast mwenyeji wa michuano hiyo kufuzu kama moja ya timu nne bora zilizomaliza katika nafasi ya tatu.

Soma pia: Ivory Coast ukingoni mwa kutolewa nje ya michuano ya AFCON

Ivory Coast watavaana na Simba wa Teranga Senegal Jumatatu ijayo, huku Morocco wakiwa na miadi na Afrika Kusini siku ya Jumanne.

Soma pia:Moroko yaichabanga Tanzania 3-0 AFCON

Tunisia nayo imepigwa kumbo na kutolewa nje ya michuano hiyo baada ya kutoka sare ya 0-0 na Afrika Kusini inayojulikana kwa jina la utani kama bafana bafana katika mechi ya mwisho ya Kundi E mjini Korhogo.