1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sölden , Austria. Watalii tisa wauwawa katika ajali.

6 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEds

Kiasi cha watalii tisa wa Kijerumani wameuwawa katika ajali ya kigari kichotembea kwenye waya katika milima ya Alps huko Austria.

Maafisa wanasema helikopta kwa makosa ilidondosha kontena lilijaa saruji katika kigari hicho katika eneo la Sölden katika jimbo la Tyrol.

Kigari kimoja kilianguka na kingine kilikuwa kinaning’inia na kuwatupa watu waliokuwamo ndani nje .

Kiasi cha watu wengine saba wamejeruhiwa, baadhi yao wako katika hali mbaya .

Uchunguzi unafanyika hivi sasa juu ya sababu ya ajali hiyo.