1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSyria

Syria yapinga ripoti ya OPCW kuhusu shambulio la 2018

2 Februari 2023

Syria imepinga taarifa ya shirika la kimataifa la kudhibiti silaha za kemikali, OPCW, kuwa jeshi la anga la nchi hiyo lilidondosha mitungi miwili ya gesi la Chlorine kwenye mji wa Douma mwaka 2018.

https://p.dw.com/p/4N24Q
Niederlande Organisation für das Verbot chemischer Waffen (OPCW) in Den Haag
Picha: ROBIN UTRECHT/picture alliance

Syria leo imepinga taarifa ya shirika la kimataifa la kudhibiti silaha za kemikali, OPCW, kwamba wachunguzi wake walipata ushahidi unaothibitisha kuwa jeshi la anga la nchi hiyo lilidondosha mitungi miwili ya gesi la Chlorine kwenye mji wa Douma mwaka 2018.

OPCW ilitoa ripoti hiyo kufuatia uchunguzi wake kwa shambulio la Aprili 7, 2018, ambapo watu zaidi ya 40 waliripotiwa kuuawa. Marekani, Uingereza na Ufaransa ziliilamu serikali ya Syria na kuanzisha mashambulizi dhidi yake.

Syria na mshirika wake Urusi zimekanusha kufanyika shambulizi lolote na kemikali. Mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa, Balozi Milad Atieh, amewaambia waandishi habari kwamba OPCW imekuwa na upendeleo kuelekea misimamo ya mataifa ya Magharibi.