1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sweden yaifunga Marekani

Halima Nyanza(ZPR)7 Julai 2011

Sweden jana ilifanikiwa kuifunga Marekani mabao mawili kwa moja, lakini hata hivyo timu hizo zote mbili bado zinaendelea na mashindano, kutokana na kushika nafasi ya kwanza na ya pili katika kundi C.

https://p.dw.com/p/11qdP
Hekaheka goliniPicha: picture-alliance/dpa

Marekani itapambana na Brazil katika awamu ya mtoano, siku ya Jumapili. Hapo jana Brazil iliweza kuifunga Guinea Ikweta mabao mawili kwa bila.

Flash-Galerie Frauen-Fußball-WM 2011 Schweden - USA
Wachezaji wa Sweden wakifurahia ushindiPicha: picture-alliance/dpa

Wakati huo huo Australia jana iliweza kuifunga Norway mabao mawili kwa bila, na kuweza kusonga mbele, ambapo itapambana na Sweden, siku ya Jumapili.