1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sweden yagundua madini adimu ya chuma yenye thamani kubwa

13 Januari 2023

Hifadhi kubwa ya madini adimu ya chuma yenye thamani kubwa na ambayo yanahitajika, miongoni mwa mambo mengine, kwa ujenzi wa magari ya umeme na mitambo ya kuzalisha nishati ya upepo, yamegundulika kaskazini mwa Sweden.

https://p.dw.com/p/4M7LS
Schweden Seltene Erden Fund/LKAB PK in Kiruna
Picha: Jonas Ekstromer/TT News Agency/REUTERS

Hifadhi kubwa ya madini adimu ya chuma yenye thamani kubwa na ambayo yanahitajika, miongoni mwa mambo mengine, kwa ujenzi wa magari ya umeme na mitambo ya kuzalisha nishati ya upepo, yamegundulika kaskazini mwa Sweden. Kampuni ya madini ya Sweden, LKAB, imetangaza kuwa zaidi ya tani milioni moja ya madini hayo ya nadra ya chuma imepatikana karibu na eneo la Kiruna, ikiwa hifadhi kubwa kabisa ya madini kuwahi kugundulika barani Ulaya.

Mkuu wa kampuni ya LKAB, Jan Moström, amesema madini hayo huenda yakaimarisha uzalishaji wa malighafi ambayo ni muhimu katika kuhamia kwenye nishati mbadala. Maström amesema ni vigumu kukadiria ukubwa wa hifadhi hiyo ya madini hayo ya nadra ya chuma ikilinganishwa na nyingine za nje ya Ulaya. LKAB ndiyo kampuni kubwa kabisa ulimwenguni ya uchimbaji madini ya chuma katika eneo la Kiruna.