1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUswidi

Sweden kuimarisha doria za mpakani

1 Agosti 2023

Serikali ya Sweden leo imesema inalenga kuimarisha doria katika mipaka yake kutokana na hali mbaya ya kiusalama kufuatia visa kadhaa vya kukidhalilisha kitabu kitakatifu cha Qur'an.

https://p.dw.com/p/4UeVq
Maandamano nchini Pakistan kupinga kuteketezwa kwa Quran nchini Sweden
Maandamano nchini Pakistan kupinga kuteketezwa kwa Quran nchini SwedenPicha: Arshad Butt/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Ülf Kristensen, amewaambia waandishi wa habari kwamba uamuzi kuhusiana na suala hilo utatolewa Alhamis.

Kristensen amesema kuwa wanaimarisha usalama wa Sweden kwa lengo la kuwazuia watu walio na mafungamano hafifu na Sweden, kuja kufanya uhalifu au kufanya vitendo vinavyokwenda kinyume na maslahi ya kiusalama ya Sweden.

Wanaume wawili wa Irak wachoma Qur'an mbele ya bunge la Sweden.

Hapo jana, wanaume wawili raia wa Irak, Salwan Momika na Salwan Najem, walikichoma kitabu cha Qur'an mbele ya bunge la Sweden. Wawili hao awali waliwahi kufanya vitendo hivyo nje ya msikiti mkuu wa Stockholm na mbele ya ubalozi wa Irak katika mji huo, vitendo vilivyolaaniwa pakubwa na kupelekea mivutano kati ya Sweden na mataifa ya Kiislamu.