1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yakwama tena makubaliano ya utawala wa kiraia

6 Aprili 2023

Makubaliano ya kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini Sudan yamecheleweshwa kwa mara nyingine na mazungumzo kati ya pande mbili za jeshi zinazohasimiana.

https://p.dw.com/p/4Pll3
Sudan Khartoum |  Abdel Fattah al-Burhan I Kusaini makubaliano
Abdel Fattah al-Burhan - Mkuu wa Jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan (katikati) na kamanda wa wanamgambo Mohamed Hamdan Dagalo (wa pili kulia) wakinyanyua hati pamoja na viongozi wa kiraiaPicha: AFP via Getty Images

Makubaliano ya kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini Sudan yamecheleweshwa kwa mara nyingine na mazungumzo kati ya pande mbili za jeshi zinazohasimiana, hatua iliyopelekea wanaharakati wanaotetea demokrasia nchini humo kuitisha maandamano ya nchi nzima.

Sherehe za utiaji saini makubaliano hayo zilipangwa kufanyika leo Alhamis na zimeahirishwa ili kutoa nafasi kwa wanajeshi kuendelea na mazungumzo ili kumaliza tofauti zao.

Kulingana na wataalamu, suala kuu ni kujumuishwa katika jeshi kwa kikosi chenye nguvu kinachoongozwa na naibu wa kiongozi wa kijeshi, Abdel Fattah Burhan, Mohamed Hamdan Daglo.

Mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba mwaka 2021 yalisambaratisha mchakato wa mpito uliokuwepo baada ya mapinduzi ya mwaka 2019, yaliyoung'owa utawala wa Omar al Bashir.