1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yakaribia kuishiwa dawa, mafuta na ngano

5 Oktoba 2021

Baraza la mawaziri la Sudan limesema kwamba taifa hilo linakaribia kuishiwa dawa muhimu, mafuta na ngano.

https://p.dw.com/p/41Gpj
Sudan Karthoum | Anti-Regierungsproteste
Picha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Hali hiyo imejiri baada ya maandamano ya kisiasa kulazimisha kufungwa kwa bandari ya Sudan, ambayo ndiyo bandari kuu ya mashariki mwa taifa hilo.

Wanachama wa kabila la Beja mashariki mwa Sudan wamezuwia barabara na kulazimisha bandari za Bahari ya Shamu kufunga katika wiki za karibuni, kupinga kile wanachosema ukosefu wa mamlaka ya kisiasa katika eneo hilo, pamoja na hali duni ya kiuchumi.

Baraza la mawaziri lilikiri kuhusu madai ya haki ya eneo hilo, na kusisitiza haki ya kuandamana kwa amani, lakini lilionya kuwa kufungwa kwa bandari ya Sudan na barabara kuu zinazounganisha upande wa mashariki na maeneo mengine ya nchi kulikuwa kunaumiza maslahi ya Wasudan wote.