1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan Kusini kupata mkopo kutoka Falme za Kiarabu

18 Mei 2024

Sudan Kusini inakaribia kupata mkopo wa dola bilioni 13 kutoka kwa kampuni moja iliyoko katika Umoja wa Falme za Kiarabu, licha ya nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta kushindwa kudhibiti madeni yake.

https://p.dw.com/p/4g1g3
Salva Kiir Mayardit | rais wa Sudan Kusini
Rasi wa Sudan Kusini Salva KiirPicha: Brian Inganga/AP Photo/picture alliance

 

Jopo hilo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa limesema kwenye ripoti yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba nakala za hati za mkopo zinaonyesha makubaliano kati ya Sudan Kusini na kampuni ya Hamad Bin Khalifa. Mkopo huo utakuwa mkubwa zaidi kuwahi kutolewa.

Mwakilishi wa Falme za Kiarabu katika Umoja wa Mataifa hakuzungumzia chochote kuhusu makubaliano hayo na amesisitiza kuwa kampuni hiyo ni ya watu binafsi.

Sudan Kusini yaafikiana na makundi ya uasi kukomesha vurugu

Sudan Kusini inakabiliwa na shinikizo kutoka Marekani na mataifa mengine juu ya kuyatekeleza kwa haraka makubaliano ya amani ya mwaka 2018 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe na inatakiwa iandae kwa uchaguzi.