1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Sudan: RSF yadai kuchukua udhibiti wa uwanja wa ndege

31 Oktoba 2023

Wakati viongozi wa pande zinazohasimiana nchini Sudan wakiwa wameanza tena kufanya mazungumzo nchini Saudi Arabia, mapigano yameendelea kushuhudiwa sehemu mbalimbali.

https://p.dw.com/p/4YDWJ
Sudan | Mohamed Hamdan Daglo
Mkuu wa kikosi cha RSF Mohamed Hamdan Daglo akiwa na wanajeshi wake.Picha: Rapid Support Forces/AFP

Wapiganaji wa wa kundi la Rapid Support Forces RSF wametangaza usiku wa jana kuwa wamechukua udhibiti wa uwanja wa ndege wa Belila uliopo jimbo la Kordofan. Kundi la RSF na jeshi la Sudan wamekuwa wakipambana zaidi katika miji ya magharibi mwa nchi hiyo ya El Obeid na El Fasher.

Katika kipindi cha miezi mitatu sasa RSF imelidhibiti eneo la mpakani la Om Dafouq na wanaripotiwa pia kuchukua udhibiti wa njia za ziada za usambazaji wa bidhaa kuelekea mji mkuu Khartoum.

Soma Mahasimu wa Sudan wakutana tena kujadili suluhu ya mzozopia: 

Marekani na Saudi Arabia zimesema mazungumzo yaliyoanza wiki iliyopita yanalenga kuleta makubaliano ya kusitisha mapigano ili kuruhusu usambazaji wa misaada ya kibinaadamu. Miezi sita ya mapigano huko Sudan tayari imesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 9,000 huku wengine karibu milioni 6 wakiyahama makazi yao.