1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Strasbourg.Bunge la Ulaya lahoji kuhusu jela za CIA barani humo.

8 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDEP

Wabunge wa Ulaya wanazitaka serikali zao zifichue habari zinazohusika na jela za shirika la upelelezi la Marekani CIA zilizo barani Ulaya.

Poland na Romania zinashukiwa kuwa na jela za aina hiyo.

Siku ya Jumatano, rais wa Marekani George W. Bush alikiri kuwa shirika la CIA liliwahoji washukiwa darzeni kadhaa waliozuiliwa katika jela za siri nn’je ya Marekani.

Aidha Bush akaongeza kuwa washukiwa 14 wamehamishwa kutoka jela hizo na kupelekwa jela ya kijeshi ya Marekani ya Guantanamo iliyopo nchini Cuba.

Mapema mwaka huu, baraza la Ulaya linalotetea haki za binaadamu, lilituhumu kuwa Poland na Romania zimekaribisha jela hizo za siri za CIA.

Hata hivyo serikali za Warsaw na Bucharest zimekanusha madai hayo.