1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier kumpa mkewe figo

Josephat Nyiro Charo23 Agosti 2010

Mwanasiasa huyo ambaye alikuwa naibu kansela na waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani katika serikali iliypoita, atajiondoka kwa muda katika ulingo wa siasa

https://p.dw.com/p/OuJR
Frank-Walter Steinmeier, kiongozi wa chama cha SPDPicha: AP

Tukibakia hapa Ujerumani,kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha kisoshalisti cha SPD,Frank Walter Steinmeier ametangaza hii leo kuwa anajiondoa katika harakati za kisiasa kwa muda ili kumpa mkewe figo moja anayoihitaji. Mke wake, Jaji Elke Buedenbender aliye na umri wa miaka 48 aliye na matatizo ya figo anahitaji figo ya dharura na hali yake ya afya imezidi kuwa mbaya katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita. Bwana Steinmeier ameamua kuwa mfadhili wake kwani wamesubiri kwa muda jambo linaloihatarisha afya ya mke wake wa miaka 15.

Thelma mwadzaya amezungumza na Profesa AbdulLatif Abdalla mhadhiri katika chuo kikuu cha Leipzig kilicho mashariki ya Ujerumani.