1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STARSBOURG:Bunge la Ulaya latoa baraka kwa mazungumzo ya Uturuki kuigizwa katika Umoja wa Ulaya.

28 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEWn

Bunge la Ulaya huko Strasbourg limetoa baraka zake kwa mazungumzo yanayohusu uanachama wa Uturuki yanayotazamiwa kuanza wiki ijayo.

Hata hivyo katika azimio lisilofungamana na upande wowote,wabunge wa Ulaya wanataka Uturuki kutambua mauaji ya halaiki ya Waarmania yaliyofanywa chini ya utawala wa Ottoman mwaka 1915,kama sharti kuu la wao kukubaliwa kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Suala hilo linaloonekana kuwa na utata,limekuwa ni kikwazo kikubwa,baada ya Uturuki kukataa kukubali mauaji ya Waarmenia milioni 1.5 kama ni mauaji ya halaiki.

Katika mkutano na waandishi habari huko Strasbourg,Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki alieleza kuwa nchi yake huenda ikajitenga na mazungumzo ya kukubaliwa,iwapo itashurutishwa kufanya jambo jingine lolote isipokuwa kupewa uanchama kamili wa Umoja wa Ulaya.