1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Starmer aelekea Downing 10

5 Julai 2024

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Labour nchini Uingereza anaelekea kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo, wakati matokeo ya mwisho ya uchaguzi uliofanyika jana yakionesha chama chake kupata ushindi wa kishindo.

https://p.dw.com/p/4htE9
Keir Starmer
Mkuu wa chama cha Labour, Keir Starmer.Picha: Kin Cheung/AP Photo/picture alliance

Keir Starmer anatazamiwa muda wowote kuanzia sasa kutangazwa kuwa waziri mkuu kuchukuwa nafasi ya Rishi Sunak, ambaye chama chake cha Conservative kimeangushwa vibaya kwenye uchaguzi huu.

Amewaambia wafuasi wake kuwa watu wa Uingereza wametowa kauli yao, muda mfupi baada ya kutangazwa kuwa amefanikiwa kukibakisha kiti chake bungeni.

Soma zaidi: Labour kuzowa viti 410, Conservative yaambulia 131 tu

Kwa ujumla, chama cha Labour kinatazamiwa kuwa na viti 410, kikifuatiwa na Conservative chenye viti 131, huku cha kiliberali, Lib Dem, kikiwa cha tatu kwa viti 61.

Haya ni matokeo mabaya kabisa kwa Conservative, kwani yamevunja rikodi ya mwaka 1906 kilipopata viti 156.