1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 37 wamekufa katika mkanyagano Brazzaville.

21 Novemba 2023

Vijana wapatao 37 wamefariki dunia kufuatia mkanyagano uliotokea usiku wa kuamkia leo wakati wa zoezi la kuwasajili makuruta wa kijeshi katika mji mkuu wa Jamhuri ya Congo.

https://p.dw.com/p/4ZGZQ

Waziri Mkuu Anatole Collinet Makosso amethibitisha tukio hilo na kusema idadi isiyojulikana ya watu wengine wamejeruhiwa. Wiki iliyopita, jeshi katika taifa hilo la Afrika ya kati pia linalojulikana kama Congo-Brazzaville, lilitangaza kuwa linaajiri watu 1,500 wenye umri wa kati ya miaka 18 na 25.Hadi sasa chanzo cha mkasa huo hakijabainika wazi, lakini mashuhuda wamesema baadhi ya watu walikuwa wakijaribu kuingia kwa nguvu uwanjani hapo, jambo lililosababisha mkanyakagano. Shirika la habari la AFP halikuweza kuthibitisha kwa uhuru maelezo hayo.