1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Spika Kificho wa Zanzibar ataka Shirikisho la Afrika Mashariki lizingatie historia

Mohammed Khelef29 Novemba 2011

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, ametaka mchakato wa kuelekea uundwaji wa Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki, kuzingatia ukweli kwamba nchi wanachama zina historia tafauti.

https://p.dw.com/p/13J6F
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.Picha: DW

Katika mahojiano haya na Mohammed Khelef, Spika Kificho, anasema ni jambo la muhimu kwa historia kuchukuwa nafasi yake, na kuzingatia ukweli kuwa nchi wanachama zina maumbile tafauti. Zanzibar ni moja ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ingawa inawakilishwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia Tanzania, kuna mambo mengi ambayo ya Jumuiya ambayo si ya Muungano.

Mahojiano: Mohammed Khelef/Pandu Ameir Kificho
Mhariri: Othman Miraji