1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Spika Jacob Oulanya atakumbukwa kivipi Uganda ?

Lubega Emmanuel 21 Machi 2022

Spika huyo aliyefariki nchini Marekani alikokuwa akipatiwa matibabu atakumbukwa kuhusika pakubwa katika siasa za Uganda ikiwemo mchakato wa mabadiliko ya katiba.

https://p.dw.com/p/48n6w
Uganda I Parlamentswahlen
Picha: Parliamentary Press Office/Uganda

Yumkini kifo cha Jacob Oulanya kilibaki siri kubwa ya serikali kwa muda usiojulikana tangu uvumi kuibuka wiki mbili zilizopita kwamba amefariki nchini Marekanin alikopelekwa kwa matibabu. Jana jumapili rais Yoweri Museveni mwenyewe ndiye alifahamisha taifa rasmi kwamba kifo hicho kilitokea jana asubuhi na alikawia kwa muda kutoa  taarifa hiyo akitaka kwanza familia yake ijulishwe.

Hiki ndicho chanzo cha mjadala kuhusu hasa ni lini alifariki na kwa nini watu mashuhuri kadhaa walidhaminiwa na serikali kwenda Marekani kumjulia hali mtu ambaye hali yake ilibaki siri.  Katika maisha yake ya kisiasa, Spika Oulanya amekuja kutambuliwa kama mtu mwenye busara katika kudhitibi joto la mijadala bungeni.

Akiwa naibu spika kwa muda wa miaka 10 aliongoza mijadala kadhaa iliyopelekea katiba ya nchi kufanyiwa mageuzi. Miongoni mwa hiyo ilikuwa kuondoa ukomo wa awamu za urais na kisha baadaye kuondoa kipengele cha umri wa mgombea urais. Mageuzi haya mawili ndiyo yamemwezesha rais Museveni kuendelea kutawala Uganda bila kukinzana na katiba.

Spika wa bunge la Uganda afariki dunia

''Oulanya alikuwa mpatanishi''

Spika wa bunge la Uganda Jacob Oulanya afariki nchini Marekani
Spika wa bunge la Uganda Jacob Oulanya afariki nchini Marekani Picha: Parliamentary Press Office/Uganda

Ni kwa ajili hii ndipo baadhi ya wanasiasa wana mtazamo kuwa marehemu Oulanya alichangia pakubwa kwa utawala wa sasa kubaki madarakani na ndiyo maana Museveni naye alifanya juu chini kuwashawishi wabunge kumchagua kuwa spika badala  ya mpinzani wake

Rebecca Kadaga ambaye inaelezewa kuwa tangu ashindwe hajawahi kukanyaga bungeni licha ya kuwa ni waziri wa masuala ya Afrika Mashariki. John Kibego ni mwanahabari na mchambuzi wa masuala ya kisiasa .Lakini pia Jacob Oulanya alionekana akijaribu  kuhakikisha usawa kati ya wanasiasa na chama tawala na wale wa upinzani.

Museven akataa mwanae kujiuzulu

Mara kadhaa alipinga vitendo vya kuwanyanyasa wanasiasa wa upinzani na aliagiza wengine waachiwe mara moja kutoka vizuizini. Kulingana na katiba, wabunge wanatakiwa kumchagua spika mwingine mara moja kabla ya kikao chochote kufanyika ikiwemo kuratibu mazishi ya marehemu. Hapo ndipo kuna

mtihani kwa wabunge kwani hii ni mara ya kwanza hili kutokea. Haijulikani kama serikali itaendelea kuwasaka na kuwakamata  watu

waliotangulia kusambaza taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba spika Oulanya alikuwa amefariki kama agizo lilivyotolewa wiki iliyopita.