1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUhispania

Spain na France kutunishiana misuli nusu fainali

9 Julai 2024

Timu ya taifa ya Ufaransa inateremka uwanjani leo mjini Munich kupambana na Uhispania katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Ulaya EURO 2024.

https://p.dw.com/p/4i4Xo
Michuano ya EURO 2024 | Robo fainali | Ureno vs Ufaransa
Mshambuliaji Kylian Mbappe akipiga shuti katika pambano dhidi ya UrenoPicha: JAVIER SORIANO/AFP/Getty Images

Mshambuliaji Kylian Mbappe ataiongoza timu yake Les Bleus dhidi ya Uhispania, ambayo ni moja kati ya timu zinazopigiwa upatu kushinda michuano hiyo.

Ufaransa hata hivyo imekosolewa kwa kuonesha mchezo usiovutia. Timu hiyo imefika nusu fainali bila ya kufunga bao katika mchezo wa wazi.

Soma pia: Watu 830,000 wakaguliwa mipakani Ujerumani kwa siku 21

Uhispania kwa upande wao itazikosa huduma za kiungo Pedri aliyepata jeraha katika mechi ya robo fainali dhidi ya Ujerumani pamoja na mabeki Robin Le Normand na Dani Carvajal aliyepigwa kadi nyekundu katika pambano dhidi ya Ujerumani.