1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

Southgate ajiuzulu kama kocha wa England

16 Julai 2024

Kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya England Gareth Southgate amejiuzulu, baada ya kushindwa na Uhispania kwa mabao 2-1 katika fainali ya Euro 2024.

https://p.dw.com/p/4iNmO
Gareth Southgate
Gareth Southgate alichukua nafasi ya kuifundisha England mwaka 2016Picha: Bradley Collyer/empics/picture alliance

Kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya England Gareth Southgate amejiuzulu, baada ya kushindwa na Uhispania kwa mabao 2-1 katika fainali ya Euro 2024.

Licha ya Kocha huyo kusifiwa kwa usimamizi wake na kuiwezesha England kufika fainali mbili, Southgate alikabiliwa pia na ukosoaji kutokana na mbinu alizokuwa akitumia.

Kocha huyo amesema yeye kama Muingereza ana fahari kubwa, na imekuwa heshima kubwa kuichezea timu ya taifa ya England na pia kuwa mwalimu wa timu hiyo. Sasa ni wakati wa kuanza ukurasa mpya katika taaluma yake.

Southgate, 53, alichukua nafasi hiyo mwaka 2016na kuiongoza Uingereza kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na fainali mbili za michuano ya Euro.