1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Soka: Ujerumani haitatishwa na Colombia

16 Julai 2023

Kiungo wa kati wa Ujerumani Svenja Huth amesema hawatatishwa na Colombia katika michuano ya wanawake ya Kombe la Dunia hatua ya makundi.

https://p.dw.com/p/4TyDw
WM Qualifikation Frauen | Deutschland-Türkei | Lea Schüller
Picha: regios24/imago images

Hii ni baada ya timu hiyo ya Amerika Kusini kushutumiwa kwamba ilitumia nguvu kupita kiasi katika mechi dhidi ya Ireland.

Siku ya Ijumaa Ireland ilijiondoa katika mechi dhidi ya Colombia dakika ya 20 ya mchezo baada ya matukio kadhaa ya kuchezwa rafu.

Soma pia: Bendera za jamii asilia kupepea kombe la dunia Australia na New Zealand

Shirikisho la soka la Ireland limesema Colombia ilitumia nguvu kupita kiasi na kocha wa timu hiyo Vera Pauw alisema wachezaji wake walihofia kuumzwa miili yao.

Kwa upande wake shirikisho la soka la Colombia limeeleza kuwa timu yake ilicheza kwa kufuata sheria za soka.

Mabingwa mara mbili Ujerumani watamenyana na Colombia katika mechi yao ya pili ya kundi H mnamo Julai 30 kwenye mashindano hayo nchini Australia na New Zealand.