1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SOFIA:Hukumu ya kifo kwa wauaji wa waziri mkuu wa zamani

28 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFwt

Mfanyabiashara wa Bulgaria na watu
wanne alioshirikiana nao wamehukumiwa kifungo
cha maisha gerezani leo hii kwa mauaji ya
mwaka 1996 ya waziri mkuu wa zamani wa nchi
hiyo Andrei Lukanov.
Mfanyabiashara tajiri mkubwa wa
shughuli za ujenzi Angel Vassilev ameshutumiwa
kwa kuamuru mauaji ya Lukanov baada ya kampuni
yake ya ujenzi Calonel kufanyiwa uchunguzi wa
mikataba ya biashara ya ubabaishaji.
Raia wa Ukraine Alexander Russov
ameshutumiwa kwa kumuuwa waziri mkuu huyo wa
zamani wakati akitoka nyumbani kwake Oktoba
pili mwaka 1996.
Washtakiwa wana wiki mbili za kukata
rufaa ya kupinga hukumu hiyo.