1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya mwisho ya kuwasilisha wagombea mwenza Kenya

16 Mei 2022

Leo ndio siku ya mwisho kwa wagombea wa urais Kenya kutangaza wagombea wenza kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti. Macho yote yameelekezwa kituo cha mikutano cha KICC katikati ya jiji kwa tangazo la mgombea mwenza wa muungano wa Azimio la Umoja unaoongozwa na Raila Odinga. Saa chache zilizopita muungano wa Kenya Kwanza ulimtangaza Rigathi Gachagua kuwa mgombea mwenza wa naibu wa rais William Ruto.

https://p.dw.com/p/4BMMw