1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSierra Leone

Sierra Leone yapiga marufuku mikutano ya kisiasa mitaani

4 Aprili 2023

Sierra Leone imepiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa mabarabarani, utamaduni ambao kwa miongo kadhaaa umeandamana na kampeni za uchaguzi, kabla kufanyika uchaguzi mkuu Juni 24.

https://p.dw.com/p/4Pg3t
Sierra Leone Wahlkampf 1
Picha: Daniel Pelz

Ikiitangaza marufuku hiyo tume inayosimamia vyama vya siasa Sierra Leone ilisema vipindi vya uchaguzi si wakati wa kucheza na kufanya sherehe, bali ni wakati wa kutafakari. Msemaji wa tume Lucien Mommoh amesema marufuku hiyo itasaidia kupunguza machafuko.

Kwa kawaida vyama viwili vikuu vya siasa nchini humo, Sierra Leone People's Party, SLPP, ambacho kiko madarakani kwa sasa, na chama cha All People's Congress, APC, hufanya mikutano kama magwaride kupitia kote mjini Freetown.

Chini ya sheria mpya vyama vinatakiwa vichague eneo moja tu kama vile uwanja wa mpira au kituo kikuu cha jamii kufanyia kampeni zao. Rais wa sasa Julius Maada Bio atawania muhula wa pili huku mpinzani wake mkuu, kiongozi wa chama cha APC Samura Kamara, akikabiliwa na mashitaka ya rushwa, ambayo huenda yakamfanya afungiwe kugombea iwapo atatiwa hatiani.