1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shule zafunguliwa Uganda baada ya miaka miwili

Lubega Emmanuel10 Januari 2022

Siku ya kwanza rasmi ya masoma nchini Uganda, huku wanafunzi, wazazi na waalimu wanashuhudiwa wakifanya kila juhudi kuhakikisha kurejea kwa hali ya kawaida.

https://p.dw.com/p/45L9T
Uganda | Schule in Kampala
Picha: Nicholas Kajoba/Xinhua/imago images

Mwalimu darasa la saba shule ya msingi ya umma ya Nakasero katikati ya mji wa Kampala. Shule hii ina wanafunzi zaidi ya elfu moja

na wameanza masomo wakizingatia kanuni zote za kudhibiti kusambaa kwa COVID-19. Miongoni mwa kanuni hizo ni kuhakikisha kuwa hakuna misongamano ya watoto sehemu yoyote na kwa hiyo wanakwenda kwa mapumziko mafupi kwa zamu. 

Kwa upande wao, wazazi wanaelezea furaha yao kwamba angalau sasa watoto watakuwa katika mazingira ambayo ni salama kwao kuliko kubaki mitaani kwani wengi wamejiingiza katika vitendo viovu  ikiwemo wengine kushiriki ukahaba na kupata mimba. Kero nyingine kwa wazazi ni bei ghali ya vifaa vya matumizi shuleni.

Wanaotakiwa kurejea shule

Kulingana na ratiba iliyotokewa na serikali, wanafunzi wa viwango mbalimbali watarudi shuleni kwa makundi ili kuepusha misongamano. Hii leo ni wanafunzi wa vidato vya tano na sita ndiyo wametakiwa kurudi pamoja na wale  katika shule za kutwa. Mwalimu Simon Muhumuza wa shule ya sekondari amesema hivi kuhusu hali walimu wakati huu wa shule kufunguliwa.

Wazazi wengi wamelezea kuwa hawako tayari kuwarudisha watoto shuleni kutokana na changamoto kadhaa za kupata ada kwani walifutwa kazi katika kipindi hicho au mapato yao kushuka. Baadhi wameamua kuwatoa watoto kutoka shule za ada za juu ambazo nyingi ni za binafsi na wameshuhudiwa wakiwasajili katika shule za serikali.