1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shughuli za uokozi zaaendelea baada ya ajali ya boti Italia

Hawa Bihoga
27 Februari 2023

Shughuli za uokoaji zinaendelea baada ya boti iliokuwa imebeba wahamiaji kugonga mwamba kwenye pwani ya Italia. Hadi sasa waokoaji wameopoa miili zaidi ya 60 huku wengine kadhaa wakiwa bado hawajapatikana.

https://p.dw.com/p/4O11U
Italien | Bootsunglück mit vielen Toten
Picha: Giuseppe Pipita/ZUMA/ANSA/IMAGO

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema wanahofia kwamba idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka hadi kufikia 100 kutokana na manusura kudokeza kwamba boti hiyo ilikuwa na abiria 200 ilipong'oa nanga Uturuki.

Waziri mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif amesema takriban wapakistan 20 ni miongoni mwa waliofariki katika mkasa huo na tayari mamlaka zinawasiliana na serikali ya Italia.

Uamuzi wa Italia unaweza kuathiri sheria za uhamiaji Ulaya?

Italia ni kituo kikuu kwa wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya kwa njia ya bahari, na takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha zaidi ya watu 17,000 wamekufa na kupotea eneo la kati la Mediterania tangu 2014. UN inakadiria kuwa mwaka huu pekee wamekufa watu 220.