1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utafutaji wa manusura wa ajali ya boti Ugiriki kumalizika

17 Juni 2023

Shughuli ya kuwatafuta walionusurika kwenye ajali ya boti iliyokuwa inawasafirisha wahamiaji katika bahari ya Mediterania inakamilika hii leo Jumamosi

https://p.dw.com/p/4Si7p
Griechenland Kalamata Schiffsunglück Überlebende
Picha: John Liakos/AP Photo/picture alliance

Walinzi wa pwani ya Ugiriki walikuwa wanaendelea na msako katika eneo hilo wakitumia manowari ya kijeshi, boti tatu za doria na helikopta, ingawa upepo mkali umekuwa ukizorotesha shughuli hiyo.

Soma pia: UN yataka uchunguzi mkasa wa kuzama kwa boti Ugiriki

Matumaini ya kuwaokoa manusura zaidi ni kama yamepotea, baada ya boti hiyo ya uvuvi iliyokuwa imefurika wahamiaji kati ya 500 hadi 700 iliyokuwa ikitokea Afrika kwenda Ulaya kuzama siku ya Jumatano. Jumla ya watu 104 waliokolewa na miili 78 ikapatikana.