1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Giza latatiza shughuli katika uwanja wa ndege wa JKIA Kenya

26 Agosti 2023

Waziri wa uchukuzi Kenya Kipchumba Murkomen, amewaomba msahama raia wa taifa hilo, baada ya umeme kukatika nchi nzima na kutatiza safari pamoja na abiria katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa JKIA mjini Nairobi.

https://p.dw.com/p/4VbdP
 Nairobi airport JKIA
Picha: Billy Mutai/AA/picture alliance

Umeme ulikatika katika sehemu zote nchini humo kuanzia saa 9.45 jana usiku. Shirika la umeme nchini humo KPLC limesema  lilipata hitilafu katika mifumo ya kusamabaza umeme, iliyosababisha umeme kukatikakatika sehemu nyingi. 

Picha za abiria waliokuwa gizani katika uwanja wa ndege zimesambaa katika mitandao ya kijamii huku mamlaka ya viwanja vya ndege nchini Kenya ikisema jenereta yake ilifeli kufanya kazi. 

Bado haijabainika wazi ni hasara kiasi gani iliyosababishwa na tukio hilo katika uwanja huo wa ndege wa JKIA unaotumiwa kibiashara na hata kitalii. Na haijajulikana pia ni safari ngapi hasa zilikatishwa kufuatia hitilafu hiyo. Umeme ulirejeshwa katika uwanja huo wa ndege saa tano baada ya  tukio hilo lakini bado baadhi ya maeneo nchini humo hayana umeme.