1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Shoigu: Urusi yasukuma vikosi vya Ukraine Magharibi

3 Aprili 2024

Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu, amesema kuwa jeshi la nchi yake linasukuma vikosi vya Ukraine kuelekea upande wa Magharibi mwa nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4eMu2
Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu
Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei ShoiguPicha: Russian Defence Ministry/dpa/picture-alliance

Shoigu amesema vikosi vya Urusi vimeteka eneo la kilomita za mraba 403 la Ukraine tangu mwanzoni mwa mwaka mpya na kudhibiti miji mitano na vijiji katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo mnamo mwezi Machi.

Zelensky apinga madai ya Shoigu

Lakini matamshi ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky pamoja na duru za jeshi la nchi hiyo, zimepinga baadhi ya madai ya Shoigu kwamba vikosi vya Urusi vimechukuwa udhibiti wa maeneo kadhaa Mashariki mwa Ukraine.

Soma pia:Ukraine yasema ilidungua droni mbili kati ya tatu za Urusi usiku

Wakati wa hotuba yake ya kila jioni kwa njia ya video, Zelensky alitaja maeneo yanayopiganiwa na vikosi vya Ukraine ikiwa ni pamoja na Tonenke lililotajwa na Shoigu, hali inayoashiria kutokuwa na uhakika wa udhibiti wa Urusi katika mji huo.

Hata hivyo madai ya pande zote mbili hayakuweza kuthibitishwa kwa njia huru.