1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SHIRIKA LA UJERUMANI LA MSAKABA MWEKUNDU LAHUDUMIA WATOTO WA NJIANI RWANDA:

Sandra Petersmann/Ahmed M. Saleh19 Novemba 2003

Tarahe 19 Novemba ni "Siku ya Kimataifa ya Haki za Watoto". Tangu 1999 Shirika la Msalaba Mwekundu la Ujerumani limekuwa likitoa misaada ya kifedha kwa Kituo cha Kuwahudumia watoto wa njiani, Rwanda. Kituo hicho kiitwacho Maison de la Jeunesse kiko mjini Rwanda.

https://p.dw.com/p/CHj4

Zaidi ya watu 800,000 waliuawa mwaka 1994 katika mauawaji ya halaiki nchini Rwanda. Wengi wa wahanga hao walikuwa watu wa kabila la Watutsi, japokuwa waliuawa pia Wahutu wengi waliokuwa na misimamo wastani. Katika muda wa siku 100 walikwisha uawa watu hao kadiri miliyoni moja katika nchi yenye wakazi miliyoni 8. Maafa hayo bila ya shaka yameibadili sura ya Rwanda. Wimbo kubwa la wakimbizi lilisababishwa na mauwaji hayo ya halaiki pamoja na vita vilivyofuatilia hiyo miaka 9 iliyopita. Akina mama waliwapoteza waume zao, majirani kuuawa wenyewe kwa wenyewe na familia nyingi zimebakia masikini wa mwisho, hadi wakabidi kuwapeleka watoto wao kwenye kutafuta kazi njiani. Peke yake katika mji mkuu Kigali inasemekana wako zaidi ya watoto 3000 wanaotapia maisha. Japokuwa tangu 1999 Shirika la Ujerumani la Msalaba Mwekundu limekuwa likisaidia kifedha kituo cha watoto hao wa njiani, lakini imedhihirika namna gani ni vigumu kuwatoa njiani watoto hao. Kwa mfano Luise mwenye miaka 16 alikuwa na miaka 7 tu baba yake alipouawa. Hii leo Luise hawezi tena kukumbuka yaliyotokea wakati ule. Anachoweza tu kukumbuka ni kuwa watu wenye silaha waliingia kijijini mwao na kuwachukua wanaume wote na kuwauwa msituni. Luise ameishi njiani miaka minne. Alikuwa akiuza vitu vya kifungia mizigo na miwa, akilazimika kutafuta mabaki ya chakula kilichotupwa. Siku za mwanzo alikuwa hurudi mara kwa mara nyumbani kwa mama yake na ndugu zake wawili wadogo wa kiume, lakini baadaye alizidi kutoweka. Leo Luise anaishi katika Kituo cha Maison de la Jeunesse kinachogharimiwa na Shirika la Ujerumani la Msalaba Mwekundu. Watumishi wa kijamii wa Kituo hicho walimmwokota njiani na kumpeleka kwenye kituo hicho. Luisi anasema anapenda kuishi hapo. Anaweza kujiosha kwa maji na sabuni na kupata nguo za kuvaa pamja na chakula. Hapo amefunzwa kusoma na kuandika pamoja na kujifunza kuwa mshoni. Shoga yake Claudine mwenye miaka 15 amepoteza wazazi wake wote wawili vitani. Mjomba wake aliwahi kuwalea yeye na ndugu zake wawili wadogo, lakini yeye alempeleka njiani kwenda kutafuta kazi. Japokuwa watumishi wa kijamii hawakupendezwa na tabia hiyo ya mjomba yake, lakini mwenyewe Claudine anasema hana mtu mwengine, amebakiwa na mjomba wake tu, kwa hivyo anajaribu kumstiri. Ameamua kwa hiyari kwenda kutafuta kazi njiani, anasema. Familia yake iliposhindwa kumpa msaada aliyopewa na wazazi wake, aliamua kwenda kutafuta kazi. Lakini daima ameendelea kuwasiliana na familia yake. Na chochote alichopata alikipeleka nyumbani kuisaidia familia yake. Alipookotwa njiani na watumishi wa kijamii, kwanza mjomba wake hakutaka kumwachilia achukuliwe na Kituo cha Maison de la Jeunesse badala ya kufanya kazi na kuchuma pesa. Lakini baadaye alikubali. Sasa Claudine amefurahi kuwa hana haja ya kutapia maisha peke yake: Ni hatari kufanya kazi katika njia ambazo zimeikwisha furika watoto wengi wanaotafuta kazi. Vijana wanawakera wasichana, na wakubwa zaidi wanawabaka. Wasichana wengi wametiwa mimba kwa nguvu, kisha wanazaa watoto wasioweza kuwahudumia. Maison de la Jeunesse kinawahudumia watoto 400 waliokotwa njiani. Hawalazimiki kuishi huko, kwani wengi wao hurudi nyumbani kulala kwa familia zao. Watoto hao hupewa chakula kimoto kutwa mara tatu. Kituo hicho huwalipia madeni yao na jioni kuwasaidia kufanya kazi zao wafanye kazi zao za shule. Wengine wanaweza kuhudhuria mafunzo ya kazi za mkono, kucheza michezo au kuwatazama wanyama wa kufuga kama mbuzi, kuku na sungura. Japokuwa wanawapa huduma hizo nzuri sana, lakini baadhi ya watoto wanawapa matatizo, anasema Mkurugenzi wa Maison de la Jeunesse, Charles Myusa. Watoto waliokuwa njiani miaka miwili, mitatu au minne hawawezi tu mara moja kujizoesha na maisha ya kawaida, kwa kuwa maisha ya njiani yamewapa uhuru wa kufanya watakacho. Japokuwa wasaidizi wa kijamii wanawajaribu kuwa na subra nao lakini mara kwa mara inawabidi wale wakali kwa sababu wengine wao wanatumia na hata kuuza vidonge vya kulevya.