1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Shirika la MSF laonya kuhusu mgogoro wa kibinadamu Nigeria

12 Machi 2024

Shirika la Madaktari wasio na Mipaka MSF limetahadharisha juu ya viwango vya kutisha vya utapiamlo na kuongezeka kwa mgogoro wa kibinadamu kaskazini magharibi mwa Nigeria.

https://p.dw.com/p/4dQr4
Waasi katika eneo hilo huvamia mara kwa mara jamii, vijiji na kufanya utekaji nyara kwa lengo la kulipwa fidia
Waasi katika eneo hilo huvamia mara kwa mara jamii, vijiji na kufanya utekaji nyara kwa lengo la kulipwa fidiaPicha: AP/dpa/picture alliance

Waasi katika eneo hilo huvamia mara kwa mara jamii, vijiji na kufanya utekaji nyara kwa lengo la kulipwa fidia, na hivyo kusababisha kile ambacho shirika la MSF limesema ni dharura ya kibinadamu iliyotelekezwa.

Shirika la madaktari wasio na mipaka limesema maafisa wa timu zake katika majimbo ya kaskazini magharibi mwa Nigeria waliwatibu watoto 171,465 wenye utapiamlo mwaka uliopita na kuwalaza 32,104 hospitali kwa utapiamlo unaotishia maisha.

Hilo ni ongezeko la asilimia 14 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.