1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la kazi duniani ILO laadhimisha miaka 100

Sekione Kitojo
11 Aprili 2019

Tangu mwaka 1919 shirika la kazi duniani ILO limekuwa likifanya shughuli zake, kwa ajili ya kuleta usawa katika maeneo ya kazi. Lakini  katika bara la Afrika kwa sasa kuna mengi ya kufanya.

https://p.dw.com/p/3GdIJ
Weinernte in Südafrika
Picha: picture-alliance/Wildlife/Harpe

Suala  la  vijana kukosa ajira  pamoja  na  wahamiaji  linatoa  changamoto mpya  kwa  shirika  hilo  la  ILO linapotimiza  miaka  100  tangu  kuundwa  kwake. Wakati  shirika  hilo  likitimiza miaka  100  tangu kuundwa  tarehe  ya  leo , bado  shirika  hilo  halijafikia  malengo  yake . 

Jordanien Bundesentwicklungsminister Gerd Müller in Kuft Sum
Maeneo ya kazi yanapaswa kuwa rafiki kwa wafanyakaziPicha: picture-alliance/dpa/A. B. Clasmann

Jana Alhamis  tarehe 11 mwezi Aprili shirika  la  kazi  duniani  ILO lilisherehekea  miaka  100 tangu  kuanzishwa. Tangu  mwanzo  kabisa mradi  huu  ulikuwa  na mtazamo  wa  dhamira  kuelekea , serikali , waajiri ,  vyama  vya  wafanyakazi  na  shirika  la  ILO  kwa  pamoja kuweka viwango vya usawa  kazini  duniani kote , na  wakati  huo  huo kuhakikisha utekelezaji  wa  hali  hiyo.

Kwa kuwa  wenye mkampuni  na  wawakilishi  wa  serikali  hawataki kabisa kushiriki katika  utekelezaji  wa  mada  hii  ya usawa wa kijamii katika  Umoja  wa  Mataifa, hali  ilivyokuwa  katika  wakati  wa   vita vikuu  vya  kwanza  ndio iliyoweza  kufanikisha  hilo. Katika  kivuli cha mapinduzi  nchini  Urusi  yanayojulikana  kama  mapinduzi  ya  Oktoba mwaka  1917  vuguvugu  la  wafanyakazi  lilipata  ushawishi  mkubwa. Bila  ya  mafanikio   ya  vyama  vya  wafanyakazi  amani  katika  bara la  Ulaya  isingekuwapo.

Kwa  hakika ILO inapaswa kutazama  kuhusu  baadhi ya  mafanikio  na mageuzi  muhimu , anasema  Benjamin  Luig kutoka Wakfu wa Rose-Luxembourg  na kukumbusha  juu  ya  kuwekwa  sheria  ya  haki  ya kukusanyika  katika suala  la  uchumi  unaohusiana  na  kilimo  mwaka 1921.

Pakistan Islamabad Kinderarbeit Straßenverkäufer Metzger
mazingira ya kazi yanapaswa kulinda afya ya mfanyakazi pamoja na mlajiPicha: DW/I. Jabeen

Mwanzoni  mwa  mapinduzi  ya  viwanda  wafanyakazi  wa  mashambani walifanyishwa  kazi  kama  watumwa, ameeleza  Luig. Pia  katika  sekta ya  kilimo  shirika  la  ILO  katika  miaka  ya  1990 mpango wake uliporomoka.

Luig anakosoa  kwamba  ILO  wakati  huo  ilitumbukia  katika  wimbi  la uliberali  mamboleo, katika  kile  kinachojulikana  kama  kuunga  mkono mpango wa kuoanisha  na  mifumo mingine  na kuuamini,  ambao unaongozwa  na  masoko.

Merkel bei der ILO
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akihutubia katika miaka 100 ya shirika la kazi duniani ILO mjini Berlin Picha: picture-alliance/dpa

Lakini  katika  miaka  iliyopita  shirika  la  ILO  lilijihusisha  zaidi  katika nyanja  ya  watoto kufanyishwa  kazi  pamoja  na  hali  ya  maeneo ya kufanyia  kazi, amesema  Luig.

Shirika la  ILO binafsi  halitapenda  kuangalia nyuma  yale  yaliyotokea katika  wakati  huu wa  maadhimisho  yake  ya  miaka  100, badala yake  linatazama  kazi  zilizoko mbele yake, linataka  mabadiliko  katika Umoja  wa  Mataifa  kuhusiana  na hali ya maeneo ya kufanyia kazi na hata Afrika , anasema  Peter Van Rooij , mkurugenzi  wa  ofisi  ya  ILO nchini  Nigeria. Ukosefu  wa  kazi  kwa  vijana  ni  changamoto  kubwa. Afrika  ni bara  changa  na mafunzo  na  elimu  ni  muhimu, ameeleza vanRooij  katika  mahojiano  na  DW.

Kwa  vijana  kuweza  kuwapa  mwelekeo  kunahitaji  mambo  mengi. Vijana  wengi  zaidi  wanakosa  kazi , mara waingiapo  katika  umri  wa kufanyakazi.

Pakistan Islamabad Kinderarbeit Armut
Kuwafanyisha kazi watoto ni changamoto kwa shirika la kazi duniani ILOPicha: DW/I. Jabeen

Matokeo  yake, wanapoaua  kutafuta  kazi vijana  wengi  kutoka  bara hilo  hukimbia  nchi  zao, idadi kubwa  wanakuwa  wakimbizi  wa kutafuta kazi.

Rooij  anasisitiza  kuwa  tunapaswa  kuwa  na  msimamo  wa  dhati katika  kufanyakazi  kwa  pamoja  na  viwanda  na  mataifa  ambayo vijana  wanakimbilia. Sio kupuuza ujuzi  wa  wahamiaji , na  kwamba  ni muhimu  kwa  baadhi  ya  nchi  kuutambua.

Vijana  ni  mtaji  wa  mabara  yote, kwa  hiyo  ILO inapaswa  kutilia maana  uwezo  wa  vijana na  kuutilia  maanani  kwa  kiasi  kikubwa,  na kuwasaidia  baadhi  ya  wale , ambao  wanataka  kujitegemea.